USAID watoa vifaa na zana za kilimo kwa Vijana 50 Iringa
19 September 2024, 7:51 pm
Na Adelphina Kutika
Shirika la marekani la maendeleo ya kimataifa,kupitia mradi wa feed the future Tanzania imarisha sekta binafsi (PSSP) limekabidhi vifaa na Zana za kilimo kwa vijana (50) wajasiriamali wanajishughulisha kilimo biashara Mkoani iringa.
Akizungumza aliyekuwa mgeni rasmi wa hafla ya hiyo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu , Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Patrobas Pascal Katambi amewataka vijana hao kuitumia fursa hiyo vizuri pamoja kutunza vifaa walivyokabidhiwa ili kujikwamua na wimbi la umasikini.
Rais wa Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) CPA Mercy Sila, Katika hotuba yake ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ngazi zote kwa juhudi zinazofanywa za kuweka mazingira wezeshi yatakayowasaidia vijana kujikwamua kiuchumi.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada amesema kama Halmashauri na Mkoa kwa ujumla watahakikisha wanasimamia pesa zinazotoka halmashauri kuu ili vijana wanufaike na pesa hizo.
Awali Mkurugenzi wa Feed the Future Tanzania Imarisha Sekta binafsi Edward Furaha amesema wamegusa zaidi vijana ili kuongeza fursa za kiuchumi pamoja na kukamilisha lengo la kisera la kuwapatia mitaji na mikopo.
Aidha mkirugenzi wa Pass Leasing Company Killo lusewa amesema kuwa lengo kuu la Pass leasing company ni kuwawezesha vijana katika sekta ya kilimo kwa kuwapatia mashine na zana za kilimo,uvuvi na ufugaji.
Kwa upande wao vijana wanaonufaika mradi wa feed the Future Tanzania chini ya ufadhili wa shirika la Marekani la Maendeleo ya kimataifa (USAID) wameshukuru mradi huo kwa kuwawezesha vifaa ambavyo vitawasaidia kujikwamua kiuchumi.
Hata hivyo Feed the Future Tanzania Imarisha Sekta binafsi ni mpango wa Kimataifa wa kudhibiti njaa na usalama wa chakula wa serikali ya marekani kwa kuzingatia wakulima wadogo hasa wanawake.
MWISHO