Nuru FM

SOS Children Villagers latoa cherehani 14 kwa wasichana Mufindi

29 August 2024, 3:15 pm

Baadhi ya watumishi kutoka SOS wakiwa katika picha ya pamoja na wanufaika wa cherehani. Picha na Joyce Buganda

Na Joyce Buganda

Shirika la SOS Childrens Villagers kupitia mradi wa binti bora limetoa vifaa vya saluni na cherehani 14 vyenye thamani ya shilingi milioni 5 na laki mbili ili kuwaendeleza wasichana hao kimaisha.

Akizungumza wakati wa zoezi la utoaji wa vifaa hivyo Mratibu wa  mradi kutoka shirika la SOS children’s villagers wilaya ya Mufindi Benson Lwakatare zoezi lililofanyika katika ukumbi wa bomani Wilayani Mufindi amesema mradi wa binti bora unajishughulisha na wasichana waliojifungua katika umri mdogo na wa nafanya kazi katika mikoa mbalimbali nchini ukiwemo mkoa wa Iringa.

Sauti ya Mratibu

Linda Salekwa ni mkuu wa Wilaya ya Mufindi ndiye aliekuwa mgeni rasmi katika makabidhiano hayo amewashukuru shirika la SOS childrens villagers kwa kusaidia serikali katika kulisukuma gurudumu la maendeleo huku akiwaasa mabinti hao kuvitunza vifaa hivyo na kutovitumia tofauti.

Sauti ya Dc

Kwa upande wake Afisa maendeleo wa mkoa wa Iringa Saida Mgeni amelipongeza shirika la SOS children’s villagers  kwa kuendelea kushirikiana na serikali kwani shirika hilo limekuwa mstari wa mbele katika jamii kama elimu mashuleni kwa kuwasaidia watoto lakini pia kwa mradi wa binti bora kunawafanya  wasichana kujua stadi za maisha kwa kupata mafunzo mbalimbali ili kujijengea stadi za kujitegemea pamoja na watoto wao waliojifungua mapema lakini pia kurudi mashuleni kuendelea na masomo baada ya kujifungua.

Sauti ya Afisa

Hata hivyo baadhi ya wasichana hao wamesema hawana cha kuwa lipa shirika hilo la SOS  kwa kuwapa vifaa hivyo na kuahidi kuvitunza vifaa hivyo ambavo vitawasaidia kuendeleza maisha yao kwa ujumla.

Sauti ya Wasichana

MWISHO