Wananchi wa Kikombo walalamikia ubovu wa barabara
23 August 2024, 10:28 am
Na Fredrick Siwale
Wananchi wa Kijiji cha Kikombo Kilichopo Kata ya Isalavanu Halmashauri ya Mafinga Mji wamelalamikia ubovu wa barabara jambo linalopelekea kuwa na vumbi linalotarisha afya zao.
Wakizungumza katika ziara ya kikazi ya Mbunge wa Jimbo la Mafinga Cossato Chumi katika Eneo lao, baadhi ya wananchi wamesema kuwa barabara imekuwa kero kwao huku wakishangaa mpaka sasa bado barabara hazijatengenezwa japo waliahidiwa zitakarabatiwa baada ya mvua kukata.
Naye Diwani wa Kata ya Isalavanu Charles Makoga amesema kuwa kulitokea mkanganyiko wa ukabarabati katika barabara hizo kwani zipo chini ya Wakala wa Barabara Tarula na wako katika utekelezaji wake.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini ambaye ni Naibu Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Cosato Chumi amesema Ukarabati wa baranara uliofanywa na Tarura Wilaya ya Mufindi katika eneo la Kikombo haukubaliki huku akiagiza hatua za haraka zichukuliwe.
MWISHO