Mtunzi: Msiwafiche watoto wenye ulemavu
19 August 2024, 9:12 pm
Tabia ya kuwaficha watoto wenye ulemavu imendelea kukithiri katika Jamii jambo lililomuibua mganga Mkuu wa Wilaya ya iringa kukemea kitendo hicho.
Na Joyce Buganda
Wazazi mkoani Iringa wametakiwa kutowaficha watoto wenye changamoto ya ulemavu kwani kwa kufanya hivyo ni kuwanyima haki zao za msingi.
Wito huo umetolewa na Mganga Mkuu wa Wilaya Iringa(DMO) Godfrey Mtunzi wakati wa zoezi la ugawaji wa vifaa kwa watoto wenye ulemavu ambavyo ni viti mwendo na baiskeli lililofanyika katika ofisi ya Lebao’s Kids Foundation iliyopo Manispaa ya Iringa ambapo amewataka wazazi waliohudhuria katika zoezi hilo wawe mabalozi kwa wengine ili watoto hao wapate haki sawa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Lebao’s Kids Foundation Theophil Myinga amesema kuwa wamekuwa wakishirikiana na wazazi wenye watoto wenye uhitaji wa kwenda katika vituo vikubwa nje ya mkoa ili kupata huduma za kitabibu.
Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya watu wenye ulemavu (SHIVYAWATA) Shaban Shomari amesema kuwa shirikisho hilo ni chombo kikuu cha vyama vyote vya watu wenye ulemavu na lengo lake ni ufuatiliaji wa mambo yote yanayowahusu watu wenye ulemavu zinafika bila kuwa namakundi.
Naye mmoja wa wazazi ambao watoto wao wamepata misaada hiyo wameshukuru kwa huduma inayotolewa kituoni hapo kwa watoto hao ambao wamekuwa wakitengwa na jamii.
MWISHO