Nuru FM

Sakata la nauli kupanda Mafinga Mji latua baraza la madiwani

15 August 2024, 10:55 am

Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mafinga Mji Reginant Kivinge akiwa katika kikao cha kujadili taarifa ya Robo nne ya Mwaka 2024. Picha na Hafidh Ally

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Barabarani Tanzania ndio yenye mamlaka ya kupandisha na kushusha nauli za usafiri wa uma jambo ambalo limekuwa tofauti katika Halmashauri ya mji Mafinga ambapo madereva ndio wametekeleza zoezi hilo.

Na Hafidh Ally

Siku chache baada ya madereva bajaji Halmashauri ya Mji Mafinga kupandisha nauli za usafiri huo bila kufuata malekezo kutoka mamlaka husika, suala hilo limetua katika baraza la madiwani wa halmashauri hiyo.

Akizungumza katika kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mafinga Mji kujadili taarifa kwa kipindi cha robo ya nne (Aprili hadi Juni 2024), Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Reginant Kivinge amesema kuwa sauala la madereva bajaji kujipandishia nauli limezua taharuki na wao hawakubaliani nalo.

Sauti ya Kivinge

Awali Diwani wa Kata ya Boma Mh. Julias Kisoma amewataka madiwani na watumishi wa halmashauri hiyo kujadili namna ya kupunguza nauli hizo ambazo zimekuwa kero kwa wananchi wao.

Sauti ya Kisoma

Kwa upande wake Afisa Biashara wa Halmashauri ya Mji mafinga Evance  Mtikile amesema kuwa LATRA ndio wenye mamlaka ya kupanga bei ya nauli ambapo wamepanga kukutana na kundi hilo tarehe 17 mwezi huu ili kutatua kero hiyo.

Sauti ya Mtikile

Nauli katika mji wa mafinga zimepanda mpaka shilingi 1200 ambapo awali zilikuwa kutoka eneo moja kwenda jingine ni shilingi mia saba jambo ambalo wananchi hawakubalani nalo.