Wakurugenzi Iringa kutenga bajeti ya program ya malezi PJT MMMAM
14 August 2024, 8:20 am
Utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ( PJT-MMMAM) unaweza kutoa suluhisho la kudumu la changamoto inayokabili mkoa wa Iringa ya ukatili wa kijinsia, lishe, afya na malezi bora dhidi ya watoto hususan walio kati ya umri wa miaka 0 hadi 5.
Na Joyce Buganda
Wakuu wa wilaya mkoani Iringa wametakiwa kuendelea kusimamia kikamilifu utendaji wa programu jumuishi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto PJT MMMAM hasa kwenye ngazi ya jamii kuhakikisha elimu hii inawafikia walengwa kwa afua zote tano.
Akizungumza katika kikao cha tathmini ya programu jumuishi ya taifa ya malezi makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto PJT MMMAM kwa ngazi ya mkoa Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa iringa Venance Ntyagundura ambae alimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Iringa amesema ni vema Wakurugenzi wa Halmashauri watenge bajeti ili kuwezesha utekelezaji wa program hii.
Aidha ni afisa ustawi wa mkoa wa iringa ambae pia ni mratibu wa PJT MMMAM kwa mkoa wa iringa Martin Chuwa amesema wanajitahidi kuwafikia makundi tofauti tofauti ili kutoa elimu kuhusu program hiyo.
Hata hivyo mwandishi kinara wa habari za watoto mkoani iringa Tukuswiga mwaisumbe amesema zaidi ya watu 1000 wamefikiwa kupitia vyombo vya habari kwa mkoa wa iringa kwa kupitia vipindi, makala na habari.
Kwa upande wao baadhi ya wadau walioshiriki kikao hicho wamesema wameshuru kupata elimu hiyo kwanin kumewafanya wakawe mabalozi na walimu kwa wenzao.
PJT MMMAM ni program jumuishi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kuanzia miaka 0 mpaka miaka 5 ambayo ina afua tano ambazo ni afya bora, malezi, lishe, elimu na ulinzi na usalama kwa mtoto.
MWISHO