Nuru FM

KKKT usharika wa Magulilwa kupinga ukatili wa kijinsia

13 August 2024, 9:58 am

Picha ya nembo ya Makanisa ya KKKT Tanzania.

Viongozi wa dini wana jukumu na nafasi kubwa katika kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii.

Na Mwandishi wetu

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa Dr. Blaston Gavile amelitaka kanisa hili kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii.

Akizungumza katika usharika wa Magulilwa jimbo la kusini Magharibi Askofu Gavile amesema kuwa kila mwanajamii anapaswa kukemea vitendo vya ukatili kwa watu wote ikiwemo ubakaji na ulawiti

Sauti ya Gavile

Katika hatua nyingine Kiongozi huyo amewaomba wakristo wote kuliombea Taifa hasa katika wakati huu wa kuelekea uchaguguzi wa serikali za mitaa pamoja na uchaguzi wa mwaka 2025 ili kupata viongozi wenye weredi wa kulitumikia Taifa.

Sauti ya Gavile

Pamoja na hayo Askofu wa kanisa la Kiinjili kiluther Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa Dr.Blaston Gavile  amewataka washarika kujikita katika kulima kilimo cha mkakati na chenye tija ili kuweza kujiongezea kipato binafsi na Taifa kwa ujumla.

MWISHO