Wananchi Kinyanambo walalamikia bei kubwa ya nauli
22 July 2024, 12:03 pm
Na Joyce Buganda
Uongozi wa Halmashauri ya Mafinga Mji umewaomba Uongozi wa Bajaji katika Mji wa Mafinga kupunguza nauli ya bajaji ambayo imekuwa kero kwa wakazi wa eneo hilo.
Hayo yamezungumzwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga, Mhe. Regnant Kivinge katika Mkutano uliofanyika eneo la Kinyanambo na kuongeza kuwa kuna haja ya kupunguza nauli hizo kutoka Tsh. 800/= kuwa Tsh. 700/= pamoja na Tsh. 1200/= kurudi kuwa Tsh. 1000/= na pindi Wanapokuwa na changamoto yoyote basi waishirikishe Serikali na sio kuamua wao pekee.
Nae Mwenyekiti wa madereva mafinga mji Ndg, Haruni Manga akijibu hoja za Wananchi kuwa Wanatamani urudi usafiri wa Hiace ili kuondoa kero hiyo, Amesema kuwa Suala la Nauli limeangalia pande zote kwani bado wapo katika Mjadala na Afisa Biashara, Serikali pamoja na Madereva.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa mafinga mji wamesema nauli za bajaji zimekuwa juu jambo linalopelekea wanatamani daladala zirudi kama ilivyo kuwa zamani.
Ongezeko la Nauli za Bajaji limejiri maeneo mbalimbali jirani ikiwemo Iringa Mjini, Makambako na Mjini Mafinga ingawa Afisa Biashara kwa kushirikiana na Serikali kupitia Mhe. Kivinge wameahidi kujadili na kufikia Muafaka wa Changamoto hiyo
MWISHO