Elimu, mitaji kikwazo kwa vijana Iringa kujikita katika kilimo
19 July 2024, 9:51 am
Vijana wanahitaji kuandaliwa vizuri ili waelewe wanalima nini, mtaji watapata wapi, watauza wapi mazao yao.
Na Naida Athanasi na Michael Mundellah
Ukosefu wa elimu ya kilimo bora na mitaji imetajwa kama sababu inayopelea vijana wengi Mkoani Iringa wasijiusishe na shughuli za kilimo.
Wakizungumza na Nuru fm baadhi ya vijana hao wamesema kundi la vijana wangepata elimu sahihi kuhusu kilimo pamoja na mitaji ingesaidia kuwaimarisha zaidi katika mapambano ya ajira.
Alfred Kalinga ni miongoni mwa wakulima ambao wanaendesha maisha yao kutokana na kilimo, amesema kuwa vijana wengi ni wavivu na wanataka mafanikio ya haraka jambo linalopelekea kujihusisha michezo ya bahati nasibu badala ya kilimo.
Kwa upande wake Afisa kilimo wa Manispaa ya Iringa Siri Nyenza amewashauri vijana kujihusisha na kilimo ili kujipatia kipato, kuboresha afya na kupata chakula cha kutosha.
MWISHO