Kabati:Utamaduni wa kimagharibi chanzo cha ukatili
18 July 2024, 9:34 am
Ukatili dhidi ya wanawake na wasichana unasalia kuwa kitendo cha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu duniani kote, ukiathiri zaidi ya wanawake na watoto milioni 1.3.
Na Hafidh Ally
Wazazi Mkoani Iringa wametakiwa kuachana na tamaduni za kimagharibi hasa mtoto kuvaa mavazi ambayo siyo stara ili kupunguza matukio ya ukatili dhidi yao.
Hayo yamezungumzwa na Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Iringa Dkt. Ritta Kabati na kuongeza kuwa miongoni mwa matukio yanayoongeza viashiria vya matukio ya ukatili ni pamoja na mavazi na tabia ya mtoto wa kike kukumbatiana na baba au mjomba.
Aidha Kabati amewataka wazazi kuwa karibu na watoto wao kwani wanaofanya matukio ya ukatili ni ndugu wa karibu huku akisisitiza kutolewa elimu katika jamii.
Kwa upande wake Diwani wa Viti Maalumu Dorah Nziku amesema kuwa wanaendea kutoa elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia huku wakiwaasa wazazi kutowalaza watoto wao na wageni.
MWISHO