DC Linda ahimiza mkakati wa kutokomeza ukatili na udumavu Mufindi
16 July 2024, 11:47 am
Kutokana na kuwepo kwa matukio ya ukatili, Wilaya ya Mufindi imeweka mkakati wa kukabiliana na changamoto hiyo ili kukuza ustawi katika wilaya hiyo.
Na Joyce Buganda
Serikali wilaya ya Mufindi imewataka wazazi na walezi Wilayani Humo kuhakikisha wanapambana na matukio ya ukatili wa kijinsia na kupambana na udumavu ili kukuza ustawi wa jamii.
Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Dkt. Linda Salekwa katika ziara ya kikazi kwenye Vijiji vya Kipanga, Ilogombe, Mapanda, Uhafiwa, na Katika Bwawa la Uzalishaji wa Umeme Kihansi na kuongeza kuwa jukumu la malezi ni la wazazi.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mapanda Obadia Kalenga amesema kuwa ziara ya mkuu wa wilaya imeleta matunda kwani wameazimia kutumia fedha za wananchi kukamilisha miradi ya maendeleo sambamba upatikanaji wa bima za afya kwa wananchi wao.
Mkuu wa wilaya ya mufindi anaendelea na ziara wilayani humo ambapo atatembelea miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
MWISHO