Nuru FM

Wapangaji Iringa watakiwa kujimbulisha kwa wenyeviti wa Mitaa

12 July 2024, 9:39 am

Miongon mwa nyumba za kupanga ambazo wananchi kutumia kupanga kwa ajili ya makazi.

Na Joyce Buganda

Wapangaji Manispaa ya Iringa wametakiwa kujitambulisha kwa wenyeviti wa Mitaa au wajumbe pindi wanapohama kutoka mtaa mmoja kwenda mwingine ili kudhibiti matukio ya uhalifu.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa mtaa wa Msichoke uliopo katika kata ya Makorongoni Manispaa ya Iringa Mohammed Makumba amesema kuwa ni muhimu kwa mpangaji kuwa na barua ya mwenyekiti wa mtaa anaotokea ili kumthibitisha.

Sauti ya Mwenyekiti

Makumba amesema kuwa mpangaji mpya katika mtaa wowote anapaswa kujitambulisha kwa mwenyekiti ili anapopata changamoto yoyote aweze kupata msaada huku akieleza kuwa wenye nyumba wanapaswa kuzingatia utaratibu huo.

Sauti ya Mwenyekiti

Kwa upande wao baadhi ya wenye nyumba wamesema wamekuwa huwa wakitoa utaratibu lakini wapangaji hawaufuati jambo linalopelekea kutokea kwa sintofahamu hizo.

Sauti ya Wenye nyumba

Nao baadhi ya ni wapangaji manispaa ya Iringa wamekiri kuwa huwa hawaendi kwa wenyeviti kujitambulisha huku wakijitetea kuwa huwa hawapewi utaratibu.

Sauti ya Wapangaji

MWISHO