Nuru FM

Serukamba aagiza hoja za CAG kufanyiwa kazi

3 July 2024, 12:17 pm

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba akizungumza katika Baraza la madiwani Kilolo. Picha na Joyce Buganda

Majukumu na wajibu wa kikatiba wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali yameainishwa katika Ibara ya 143 ya Katiba ya Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na Kifungu Na. 10(1) cha Sheria ya Ukaguzi, Sura ya 418.

Na Joyce Buganda

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba ameiagiza  halmashauri ya wilaya ya kilolo kuhakikisha hoja  na mapendekezo yote ya miaka ya nyuma ya mdhibiti na mkaguzi  mkuu wa hesabu za serikali CAG mpaka hesabu inayoishia June 30 2024 yanafanyiwa kazi ipasavyo.

Akizungumza katika baraza la madiwani la kujadili hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu wa serikali CAG katika halmashauri ya wilaya ya kilolo Serukamba amesema  halmashauri   iongeze  wigo Katika ukusanyaji wa mapato pamoja na kuwachukulia hatua watumishi  watakaobainika katika ubadhirifu wa fedha  zinazoletwa katika miradi,

Sauti ya RC Iringa

Serukamba ameongeza na kusema halmashauri ihakikishe inatenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya mikopo ya makundi maalumu  ambayo ni wanawake, vijana  na  watu  wenye ulemavu ili halmashauri iendelee kuwa juu pia halmashauri ihakikishe inaaongeza nguvu katika kumalizia miradi.

Sauti ya RC

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya kilolo Anna Msola amesema wameyapokea maagizo yote waliopewa na watashirikiana na watendaji wote wa halmashauri  na mkoa  kwa ujumla pia wanaomba mkurugenzi kuisimamia  idara ya afya iwe na vielelezo kwani wamekuwa wakifanya uzembe na kusababisha hoja kutokamilika.

Sauti ya Msola