Omoti: Msipandishe nauli kwa wanafunzi
3 July 2024, 8:42 am
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imesema itawachukulia hatua za kisheria mabasi yanayotoa huduma ya usafiri kwa wanafunzi kuacha tabia ya kupandisha nauli.
Na Godfrey Mengele
Kampuni za Usafirishaji Abiria Mkoani Iringa zimetakiwa kutopandisha nauli kipindi hiki ambacho shule zimefunguliwa ili kuepukana na faini.
Akizungumza na kituo hiki Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya usafiri wa Ardhini Latra Mkoa wa Iringa Joseph Omoti amesema kuwa wingi wa abiria au kuongeza kwa wahitaji wa usafiri isiwe sababu ya kukiuka bei elekezi zilizowekwa na mamlaka hiyo
Aidha Omoti amezikumbusha shule kuzingatia taratibu wanazopaswa kuzifuata katika vyombo vyao vya moto kipindi hiki shule zikiwa zimefunguliwa.
Pamoja na Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya usafiri wa Ardhini Latra Mkoa wa Iringa Joseph Omoti amezitaka shule zinazo wakusanya watoto na kuwachukua kwa magari binafsi kuhakikisha madereva kupitia vyombo hivyo wanakuwa na kibali cha kusafirisha abiria.
MWISHO