Nuru FM

Miradi ya bil.145.2 Wilaya ya Iringa kukaguliwa na mwenge wa uhuru

24 June 2024, 4:11 pm

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Kheri James akizungumza na wanahabari kuhusu ujio wa mwenge wa uhuru. Picha na Adelphina Kutika

Mwenge wa uhuru hutumiwa na Viongozi wa serikali kukagua Miradi ya maendeleo ambapo Wilaya ya Iringa utakagua Miradi ya kinaendelea upatayo 21.

Na Adelphina Kutika

Mwenge wa uhuru unatarajia kuzindua miradi 21 yenye thamani ya shiringi billion 145.2 katika wilaya iringa.

Akizungumza na vyombo vya habari Mkuu wa wilaya Iringa Mhe. Kheri James ofisini kwake , amesema Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuwasili Katika wilaya Iringa Juni 25,2024 ukitokea wilayani  kilolo ambapo utazinduaa miradi yenye thamani ya zaidi ya bilioni 145.2 na utakimbizwa kwenye Halmashauri za wilaya ya Iringa.

SAUTI YA DC KHERI

Aidha Mhe. Kheri James amewataka wananchi wote kujitokeza kwa wingi kuupokea kwani utatoa fursa  kwenye miradi na maeneo ya mikesha kupata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa hapa nchini.

SAUTI YA DC KHERI

Hata hivyo Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru wa Mwaka 2024 inasema “Tunza Mazingira, na shiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa ujenzi wa taifa Endelevu”

SAUTI YA DC KHERI