Nuru FM

Wananchi Ilangamoto walia na kero ya Umeme

12 June 2024, 9:39 am

Mradi wa umeme Mjini Makambako. Picha kwa msaada wa Mtandao

Licha ya kupatiwa huduma ya umeme katika eneo lao wananchi wa Ilangamoto wamelalamikia umeme huo hutokuwa na nguvu za kuhudumia wananchi wa eneo lote.

Na Mwandishi wetu

Wananchi wa mtaa wa Ilangamoto Kata ya Lyamkena Halmashauri ya Mji wa Makambako wamelalamikia kitendo cha kupata umeme mdogo kwa miaka mitatu sasa hali inayosababisha kukosa umeme kuanzia saa moja kamili jioni hadi saa nne usiku.

Wananchi hao wamesema licha ya kufikishiwa huduma ya umeme katika eneo lao bado umekuwa hauna msaada kwao jambo linalopelekea vyombo vyao hasa Televisheni na radio kuungua huku wakilitaka shirika la umeme Tanesco kutatua adha hiyo.

Sauti wananchi Makambako

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Ilangamoto Thomas Kiwale amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kueleza kuwa ameshaifikisha kwenye ofisi za shirika la umeme Makambako.

Sauti ya Mwenyekiti

Naye Diwani wa kata ya Lyamkena Salumu Mlumbe amesema licha ya eneo hilo kupata umeme mdogo bado kuna maeneo mengine ya mtaa huo na kata yake kwa ujumla hayajafikwa na huduma hiyo.

Sauti ya Diwani

Kwa upande wake Meneja wa Shirika la umeme Wilaya ya kitanesco Makambako mhandisi Amina Ng’imba amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kueleza kuwa shirika lipo kwenye mpango wa kupata transfoma ili kutatua changamoto hiyo.

Sauti meneja TANESCO

MWISHO