Manispaa ya Iringa kuendesha kliniki ya kutatua migogoro ya ardhi
12 June 2024, 9:45 am
Mara nyingi migogoro midogo midogo ya ardhi isiposhughulikiwa kikamilifu na dalili zake kupuuzwa hugeuka kuwa migogoro mikubwa jambo lililopelekea Halmashauri ya manispaa ya Iringa kuanzisha kliniki ya ardhi kwa wakazi wake.
Na Adelphina Kutika
Wananchi wa kata ya Nduli Halmshauri ya Manispaa ya Iringa wametakiwa kurasimisha ardhi ili kumaliza migogoro ya ardhi inayojitokeza katika kata hiyo.
Agizo hilo limetolewa na mstahiki meya Ibrahimu Ngwada Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Iringa katika uzinduzi wa kliniki ya ardhi inayondelea katika kata ya Nduli ambapo pamoja na kutatua migogoro ya ardhi , wananchi pia wamekabidhiwa hati za umiliki wa ardhi watakazotumia katik shughuli mbalimbali za maendeleo.
Kwa upande wake Afisa ardhi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Abenance Kamomonga amesema kuwa changamoto waliyoibaini katika kliniki hiyo ni uelewa mdogo wa elimu ya urasimishaji ardhi hali inayopelekea wananchi kuwa na malalamiko na sio migororo.
Nae diwani wa kata ya Nduli Bashiri Mtove ameomba vipande vyote vipimwe pamoja na kurasimisha ili kuondoa migogoro katika kata hiyo.
MWISHO