One Acre Fund yatoa miti mil 2.6 Nyanda za Juu Kusini
7 June 2024, 12:41 pm
Upandaji na uwepo wa misitu katika jamii zetu unachangia asilimia 47 ya akiba ya hewa ukaa ya misitu duniani na hutoa asilimia 60 ya miti ya mbao inayotumiwa viwandani duniani.
Na Joyce Buganda
Zaidi ya miti milioni 2 na laki 6 imesambazwa na kupandwa kutoka kampuni ya One Acre Fund kwa wakulima wa mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya na Songwe katika msimu wa mwaka 2023 na 2024 ili kutunza mazingira na kukuza kipato.
Akizungumza wakati walipowatembela wakulima katika kijiji cha utengule kata ya Ihimbo wilaya ya Kilolo Afisa Habari kutoka kampuni ya One Acre Fund Dorcas Tinga amesema kwa kipindi cha miaka mitatu wakulima ambao watatunza miti yao vizuri watapewa motisha kwa kila mti.
Aidha Christina mgata ambae ni Afisa Carboni wa kampuni ya ONE ACRE FUND amesema mradi huo unatoa miti ya aina nne pia miti hiyo ina faida nyingi ikiwemo kurutubisha udongo.
Hata hivyo baadhi ya wakulima wamesema wanaishukuru kampuni hiyo kwa kuwapa mafunzo pamoja na miti kwani kumewafanya wawe walimu kwa wenzao.
Awali mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba wakati akiongea na viongozi wa kampuni ya ONE ACRE FUND aliwashukuru kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha kilimo mseto ambacho ni rafiki wa mazingira pamoja na kutoa elimu ambazo zinasaidia kuhifadhi mazingira na kurutubisha udongo.
MWISHO