Nuru FM

Msigwa apinga ushindi wa Sugu Kanda ya Nyasa

4 June 2024, 10:29 am

Mgombea wa uenyekiti Kanda ya Nyasa Peter Msigwa akizungumzia kuhusu nchakato wa uchaguzi. Picha na Hafidh Ally

Mchakato wa kumpata Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa umemuibua aliyekuwa Mgombea wa nafasi hiyo Peter Msigwa akisema haukuwa wa haki.

Na Hafidh Ally

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa, Mch. Peter Msigwa, amekata rufaa kupinga matokeo ya uchaguzi uliompa ushindi Joseph Mbilinyi (SUGU) kwa madai kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa kanuni za katiba katika upigaji kura pamoja na kufanyika kwa fujo ambazo zilichangia kuharibu uchaguzi huo.

Msigwa amesema  katika uchaguzi huo kulikuwa na mambo mengi ambayo ni kinyume na uchaguzi za chama cha hicho ikiwa ni pamoja na wapiga kura kuitwa nje  kushawishiwa kumchagua Sugu kwa madai ni maelekezo kutoka kwa Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Freeman Mbowe.

Msigwa amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Kihesa Kilolo mjini Iringa  kuwa kama chama hicho kitashindwa kufanyia kazi barua yake ya kukata rufaa kitashindwa kujitofautisha na chama cha mapinduzi (CCM) katika swala la uminyaji wa demokrasia na haki.

Sauti ya Msigwa

Katika hatua nyingine Msigwa amekishauri chama hicho kijitafakari upya na kurudi katika misingi yake ya haki na demokrasia kwa kuheshimu mawazo ya watu wote wakiwemo wanachama wao bila kuwapinga na kuwapuuza kwani kupishana kwa hoja ndiyo ukomavu wa kisiasa.

Aidha amekanusha madai ya yeye kuhama CHADEMA na kusema kuwa kamwe hawezi kuhama chama hicho na kwamba ataendelea kupambana ndani ya chama hicho huku akiwaambia wale wote waliokuwa wanatarajia atatangaza kuahama chama hicho wataondoka wao na kumuacha yeye.

Sauti ya Msigwa

Katiba ya CHADEMA inafafanua vizuri wanaopaswa kupiga kura, makatibu wa yale mabaraza baada ya kupiga kura maana yake mwenyekiti wa vijana, mwenyekiti wa wanawake na mwenyekiti wa wazee wana makatibu.

 Waliosimamia uchaguzi huu waliwazuia makatibu kupiga kura kinyume na katiba, kwa hiyo nimekata rufaa kwenye chama changu kwamba hao ambao walipaswa kupiga kura ambao ni makatibu walizuiliwa kupiga kura, makatibu watatu wa mabaraza, kwa hiyo ukiangalia kura zilizongezeka za kwangu zilikuwa sita, watatu hawakuruhusiwa kupiga kura.