Nuru FM

RC Serukamba ahimiza usimamizi wa miradi ya maendeleo

3 June 2024, 9:45 am

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba akitoa maagizo juu ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.Picha na Joyce buganda

Mkoa wa Iringa ni miongoni mwa mikoa iliyoingiziwa fedha za miradi ya maendeleo huku wasimamizi wakitakiwa kusimamia miradi hiyo kwa weledi.

Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mkoani Iringa wameaswa kusimamia ipasavyo miradi ya maendeleo ili iwe na tija kuilingana na thamani ya fedha zinazotekeleza miradi hiyo.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani cha robo tatu ya mwaka wa fedha 2023/2024 na kubainisha kuwa moja halmashauri hiyo imeingiziwa fedha nyingi za miradi ya maendeleo lakini bado ipo nyuma katika utekelezaji wake.

Sauti ya Rc Iringa

Aidha Serukamba amesema kuwa awali halmashauri hiyo ilikuwa haifuatilii miradi kwa ukamilifu kutokana na changamoto alizokuwa nazo Mkurugenzi aliyepita hivyo kumtaka mkurugenzi wa sasa Robert Masunya kuwatumia wataalam katika miradi yote inayoendelea na kuwataka madiwani kusimamia ipasavyo

Sauti ya Serukamba

Aidha Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Steven Mhapa amesema baraza hilo limepokea maelekezo na yatafanyiwa kazi kwani miradi inapaswa itekelezwe kwa wakati hivyo kwa niaba ya madiwani watatoa ushirikiano kwa wataalamu ili kuikamilisha miradi hiyo.

Sauti ya Mhapa