DC Kheri ahimiza kuongeza nguvu katika malezi ya watoto
27 May 2024, 10:33 am
Wazazi wameshauriwa kutenga muda wa kukaa na watoto wao na kujenga mahusiano mazuri ya kirafiki na ya ukaribu ili kuwaweka karibu watoto na kuwafanya wawajue wazazi wao vizuri.
Na Adelphina Kutika
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Kheri James amewahimiza wananchi kuhakikisha wanaunganisha nguvu katika malezi ya watoto wote katika jamii zinawazunguka ili kulinda ustawi wao na kutimiza ndoto zao.
DC Kheri ameyasema hayo katika hafla ya kukabidhi vyakula katika familia (49) vilivyotolewa na Kituo cha (FISCH) Future For Iringa Children Manispaa ya Iringa wakati akizungumza na wananchi , watoto na viongozi wa kituo cha FISCH .
Awali akiwasilisha taarifa mbele ya mgeni rasim Mnufaika wa kituo cha FISCH na Mkurugenzi Wa kituo cha FISCH Alexanda Joseph Magelanga amesema wana jumla ya wanafunzi wapatao 34 ambao wanapata elimu ya vyuo vikuu na vyuo vya kati ikiwemo ufundi.
Kwa upande wao baadhi ya wazazi waliofika katika hafla hiyo Joyce Rashidi Mkonjela na Elizabeth Kisoma wamekishukuru kituo hicho kwa kuwahudumia watoto wao na kupata fursa ya kupata elimu ili kutimiza ndoto zao kutokana na mazingira magumu walionayo wazazi hao.
Yusuphu Emmy Longole ni mmoja wa watoto wanaonufaika na kituo cha fisch ameeleza namna anavyosaidiwa ili kutimiza ndoto zake.
MWISHO