Shirika la SOS kuweka usawa malezi na makuzi ya Mtoto Iringa
24 May 2024, 1:49 pm
Malezi na makuzi Bora kwa mtoto imetajwa kuwa sababu inayopelekea kuongeza kujiamini kwa watoto Mkoani Iringa
Na Joyce Buganda
Shirika la SOS children’s villagers wamefanya kikao cha kujadili na kushawishi ongezeko la bajeti katika shuhuli za ulinzi wa mtoto huku lengo kubwa likiwa kuweka usawa katika malezi na makuzi ya watoto.
Akizungumza katika kikao kilichowajumuisha madiwani wa halmashauri ya mafinga mji, na idara ya ustawi wa jamii wa halmashauri hiyo Meneja Mradi wa shirika la SOS children’s villagers Mkoa wa Iringa Bw. Victor Mwaipungu amesema shirika la SOS lilianza mda mrefu na mpaka sasa lipo katika nchi 135 duniani kote na kwa Mkoa wa Iringa shirika hilo lilianza mwaka 2016 kwa mwaka huo lilianza na mradi wa elimu.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa jamii wa halmashauri ya Mafinga mji Stella Mbeye amesema kwa upande wa Mafinga mji walijitahidi kuifikia jamii kwa kufanya vipindi vya redio zaidi ya 8, kufanya mikutano na wazazi, kwenda mashuleni kutoa elimu kujumuika katika maadhimisho mbalimbali kama siku 16 za kupinga ukatili na siku ya mtoto wa afya kwa upande wa watoto
Peter Ngusa ni Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Mafinga mji amesema suala la kuongeza bajeti kwa ulinzi na usalama wa watoto ni la muhimu lakini pia watakaa na madiwani katika vikao vyao ili kujadili suala hilo ili kulipeleka mbele zaidi Taifa la watoto.
MWISHO