Nuru FM

Matumizi ya kompyuta katika kufundishia yaongeza ufaulu Iringa

14 May 2024, 10:19 am

Mkuu wa wilaya ya Mufindi Dkt Linda Salekwa akizungumza kwenye jukwaa la Tehama lililoandaliwa na shirika la Lyra in Africa. Picha na Adelphina Kutika

Matumizi ya Kompyuta yameongeza ufanisi katika ufundishaji Hali inayochangia kuongeza ufaulu kwa wanafunzi Mkoani Iringa.

Na Adelphina Kutika

Mfumo wa kutumia teknolojia ya Kompyuta katika kufundishia mashuleni umeonesha ni mfumo unaorahisisha  ufundishaji na kukuza  hamasa kwa wanafunzi ya kupenda kusoma zaidi

Hayo yamezumzwa kwenye jukwaa la Tehama kwenye elimu lililofanyika katika ukumbi wa Sunset Mkoani Iringa na Mkuu wa wilaya ya Mfindi Dr Linda Selekwa amewataka wakuu wa shule za sekondari 10 zilizo na mradi wa Edtech chini ya ufadhili wa shirika lisilo kiserikali Lyra in Afrika mkoani Iringa kuhakikisha wanasimamia ipasavyo mradi huo  ili kutowakatisha tamaa  wafadhili wa mradi huo na kuongeza uwekezaji zaidi.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya

Kwa upande wake Mshauri wa shirika la Lyra in afrika Tanzania Diana Nisiima amesema lengo la forum hiyo ni  kutengeneza mkakati utakaosaidia kuendesha mradi katika shule hizo husani kutengeneza vifaa vitakavyoharibika na kuweka somo la ICT katika ratiba  ya vipindi vya shule .

Sauti ya Diana

Afisa Taluma Mkoa wa Iringa  Willbard Yanga amesema kuwa kupitia mradi huo wa digital umekuwa chachu ya kuongeza ufahulu mashuleni ambapo kwa matokeo ya mwaka jana darasa la saba walifaulisha kutoka  asilimia 89 – 91.5,kidato cha nne 92-94, na kidato cha sita 99-99.

Sauti ya Afisa Taaluma

Kwa upande wake mkuu wa shule Ifwagi Grace Kinyunyu  na Mwanafunzi Jasmine Kihwelo kutoka Nyang’oro sekondari wamesema kwa sasa utoro umepungua kutoka na wanafunzi kulipenda somo la ICT shuleni hapo.

Sauti ya Mwalimu na Mwanafunzi

Jumla ya kompyuta 33 zimetolewa na shirika la Lyra in Africa ambazo ni Mseke sekondari,Mlowa sekondari,Ilambilole sekondari,Ifwagi sekondari,Mazombe sekondari,Lulanzi Sekondari,Maduma sekondari,Nyang’oro sekondari na lundamatwe sekondari

MWISHO