DC Kheri: TRAMPA tunzeni siri za serikali
8 May 2024, 12:33 pm
Watunza kumbukumbu za Mamlaka za Serikali wametakiwa kudhibiti uvujishaji wa siri na nyaraka za serikali wanapotekeleza majukumu yao.
Na Adelphina Kutika
Wanataaluma wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) wametakiwa kuzingatia miiko ya taaluma yao hususan utunzaji siri za Serikali na kufuata utaratibu rasmi wa utoaji taarifa.
Agizo hilo amelitoa Mkuu wa wilaya ya Iringa ,Kheri James kwa niaba ya Mkuu wa mkoa ,wakati akifungua mafunzo na kikao kazi maalumu kwa Wanataaluma wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) kutoka Tanzania bara na Visiwani yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Masiti Mkoani Iringa ambapo amewahimiza kuwa waaminifu mahala pa kazi.
Awali, Mwenyekiti wa TRAMPA, Devotha Mrope akiwasilisha risala mbele ya mgni rasmI ametumia fursa hiyo kueleza lengo la mafunzo hayo ni pamoja na kuwajngea uwezo na kuongeza tija na ufanisi katika utendaji kazi wao.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo bi Dorkasi Brown na Atha Jonathan Kasongo wamelezea suala la utunzaji wa siri limekuwa ni changamoto kwa baadhi ya wanataaluma hao hivyo kupitia mafunzo hayo ni yatasaidia kudhibiti mianya hiyo.
MWISHO