Mgomo wa daladala Iringa waingia siku ya pili
7 May 2024, 8:35 pm
Mgomo wa madereva daladala umechukua sura mpya baada ya madereva hao kutotoa huduma ya usafiri kutokana na Madereva bajaji kuingilia Njia zao.
Na Hafidh Ally
Madereva daladala katika kituo cha stand ya zamani ya mabasi Manispaa ya Iringa wameendeleza mgomo wa kutoa huduma ya usafiri kwa siku ya pili.
Wakizungumzia sababu ya kufanya Mgomo huo, baadhi ya madereva daladala wamesema kuwa kumekuwa na tabia ya madereva bajaji kuingia katika kituo chao na kuchukua abiria kinyume na makubaliano waliyowekeana.
Kwa upande wao baadhi ya abiria manispaa ya iringa wamesema kuwa mgomo wa daladala unawafanya watumie gharama kubwa wanaposafiri.
Nao baadhi ya madereva Bajaji manispaa ya iringa wamesema kuwa mgomo wa daladala imekuwa fursa kwao na wanaweza kutoa huduma ya usafiri bila changamoto.
MWISHO