Nuru FM

DED Mafinga mji akagua miradi ya maendeleo

3 May 2024, 11:07 am

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi, Fidelica Myovella akikagua Miradi ya maendeleo. Picha na Sima Bingilek

Katika utekelezaji wa Miradi ya maendeleo, Mkurugenzi wa Mafinga mji ameamua kufuatilia utekelezaji wake ili kukamilisha kwa haraka.

Na Sima Bingilek

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi, Fidelica Myovella akiwa na baadhi ya Wakuu wa Idara ametembelea Miradi ya Maendeleo ili kufanya ufuatiliaji wa karibu wa Miradi hiyo katika Halmashauri ya Mji Mafinga.

Miradi iliyofuatiliwa na Timu ya Menejimenti ni pamoja na Zahanati ya Matanana kukagua ukamilishaji wa jengo la Maabara, Ufuatiliaji shamba la parachichi makalala, Ufuatiliaji katika Shule ya Sekondari Saohill na ukamilishaji wa maabara, Ujenzi wa madarasa mawili na Ofisi moja Shule ya Msingi Mtula, Mradi wa Ujenzi wa jengo la kuhifadhia Miili Katika Kituo cha Afya Bumilayinga, Hatua ya uwekaji wa malumalu na Mradi wa mwisho ni Ujenzi wa Madarasa mawili katika Shule ya Msingi Bumilayinga.

Akiwa katika ziara hiyo ya kufanya ufuatiliaji katika Miradi ya Maendeleo amewapongeza wanaosimamia Miradi kwa kuendelea kuikamilisha na thamani ya fedha na utekelezaji wa Miradi unaonekana.

“ Tuhakikishe tunawasimamia mafundi kwa ukaribu tushinde huku kwenye miradi kwa kufanya hivi Miradi yote itakamilika kwa wakati na tuhakikishe Mazingira yanayozunguka Miradi yanakuwa nadhifu na kutunza Mazingira “ Bi Fidelica Myovella Mkurugenzi Mji Mafinga.

Katika Ziara hiyo ya kufanya ufuatiliaji Mkurugenzi ameongozana na Mhandisi wa Mji, Afisa Kilimo na Mifugo, pamoja na Afisa Mipango.