Chadema wadai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi
3 May 2024, 11:15 am
Katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 imekuwa ni ajenda kuu katika majukwaa ya siasa hapa Nchini.
Na Joyce Buganda
Ili kupata viongozi bora Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimetaka kuwe na Tume huru ya uchaguzi na katiba mpya.
Hayo yamezungumzwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Taifa Tundu Lissu katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya mwembetogwa ambapo kabla ya Mkutano huo yalifanyika maandamano kutoka Mwangata Hadi viwanjani ambapo kwa kutembea takribani kilomita 4 ambapo Lisu amesema kuwa Chadema inataka katiba mpya ili chaguzi za mwaka huu na mwakani zifanyike kwa haki na zisitoke hujuma kama zilizotokea katika chaguzi zilizopita.
Naye Mwenyekiti wa Chadema kanda ya Nyasa Peter Msigwa amesema wao kama chadema wana maono ya kuipeleka nchi katika sehemu nzuri.
Msigwa kasema kuwa katiba ya sasa inapaswa kubadilishwa au kufanyiwa marekebisho ili kupisha uchaguzi kwani katiba hii inampa Mamlaka makubwa Rais hasa kwa Viongozi ambao wanasimamia uchaguzi hivyo kuweka mazingira magumu katika chaguzi kwa vyama vingine.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Iringa William Mungai amesema ikitengenezwa katiba mpya kila kitu kitakuwa wazi katika chaguzi zote zijazo.
MWISHO