Iringa watakiwa kutumia dawa kwa kufuata ushauri wa wataalam wa afya
24 April 2024, 10:14 am
Kutofuata ushauri wa wataalamu wa afya katika matumizi ya dawa Husababisha magonjwa kama ugonjwa wa figo, Ini na usugu wa ugonjwa.
Na Joyce Buganda
Wananchi wa Manispaa ya Iringa wametakiwa kutumia dawa kwa kufuata ushauri wa wataalamu wa afya ili kuepukana na madhara.
Hayo yamezungumzwa na Daktari wa magonjwa ya ndani kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa iringa Dokta Ryoki Mwita na kuongeza kuwa mgonjwa anaekunywa dawa tofauti na maelekezo ya mtaalam wa afya anaweza kupoteza maisha.
Hata hivyo Daktari Mwita ametoa ushauri kwa wananchi wote kuzingatia matumizi sahihi ya dawa kulingana na maelezo ya wataalamu.
Kwa upande wao baadhi ya Wananchi wa Manispaa ya Iringa wamekiri kutumia dawa bila kufuata ushauri wa wataalamu wa afya kutokana na kusahau kufuata ratiba ya dawa.
MWISHO