Wagonjwa 800 Iringa wamepata huduma katika kambi ya Madaktari Bingwa
22 April 2024, 1:46 pm
Katika kupambana na Magonjwa mbalimbali, Hospital ya rufaa Mkoa wa Iringa iliandaa Kambi ya kuwahudumia wananchi wenye changamoto za kiafya.
Na Adelphina Kutika
Zaidi ya Wagonjwa 800 wamepata huduma ya kibingwa kutoka Kambi ya Madaktari Bingwa kutoka JKCI ijulikanayo Kama Samia Suluhu Hassan Outreach Program katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.
Akizungumza Mara baada ya kumalizika kwa kambi hiyo Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani Faith Kundi amesema kambi hiyo imekuwa na mafanikio makubwa kwani imehudumia wananchi 800 , Watoto 21 waliokutwa na changamoto za kifya na Wananchi 200 ni wapya ambao walikuwa hawatambui Kama wananaradhi ya magonjwa ya Moyo.
Aidha Dr Kundi amewashauri wananchi kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza katika maeneo yao hasa za kupima afya ili kujua Hali zao za afya kabla matatizo hayajawa makubwa na kutumia muda mwingi na rasilimali fedha nyingi katika Kujitibia.
Naye daktari Bingwa wa watoto kutoka Taasis ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) Theopholl Ludovic amesema kwa upande wa watoto wamehudumia watoto 21 ambao wengi walikuwa na changamoto za shida kwenye kuta za Moyo,matundu kwenye moyo,kutanuka kwenye kuta za Moyo.
Kwa upande wake Afisa lishe kutoka Taasis ya Moyo ya Jakaya Kikwete Husna Yassin Faraji amesema asilimia kubwa ya wananchi waliogundulika kuwa na magomjwa yasiyo ambukiza walikuwa na uzito mkubwa .
MWISHO