Wananchi wa Wangama Iringa wanakabiliwa na adha ya usafiri
16 April 2024, 10:14 am
Licha ya serikali kuweka kipaumbele katika ujenzi wa miundombinu ya barabara, dado wananchi wa Kijiji cha Wangama wanakabiliwa na changamoto ya usafiri.
Na Fabiola Bosco
Wananchi wa kijiji cha Wangama kata ya Luhota halmashauri ya wilaya ya Iringa wanakabiliwa na changamoto ya usafiri hali inayopelekea kushindwa kusafirisha mazao wanaozalisha pamoja na kutumia gharama kubwa.
Wakizungumzia adha hiyo baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamesema kuwa wanapitia changamoto ya usafiri kwani wanatumia kilomita 15 kutembea mpaka kuufikia uafiri wa umma hivyo wanaiomba serikali kuwasaidia katika changamoto hiyo.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Luhota Bruno Kindole amesema idadi ndogo ya watu wanaosafiri katika kijiji hicho ndiyo sababu inayopelekea kutokuwepo kwa usafiri licha ya kutengwa kwa fedha kwa ajili ya uboreshaji wa barabara katika kata hiyo.
Uwepo wa miundombinu mizuri katika kili kata ni kichocheo cha maendeleo katika vijiji mbalimbali hapa nchini kwani bila usafiri na miundombinu bora itapelekea wananchi kuingia katika wakati mgumu wa kusafirisha bidhaa wanazozalisha.