Madaktari bingwa kutoka JKCI kuweka kambi Iringa
16 April 2024, 10:09 am
Serikali imefanya jitihada za kukabiliana na Magonjwa yasiyoambukiza kwa kuwaleta wataalamu kutoka Taasisi ya JKCI Mkoani Iringa kuweka Kambi ya kuwahudumia wakazi wa Mkoa huu.
Na Adelphina Kutika
MAMIA ya Wananchi kutoka maeneo mbalimbali mkoani Iringa wamejitokeza kwa wingi kwenye kambi ya Huduma za Madaktari Bingwa kwa Uchunguzi wa magonjwa moyo kutoka taasisi ya moyo (JKCI) .
Akizungumza na vyombo vya habari Dr Scholastica Malangalila Kaimu Mganga Mfawidhi Iringa amesema Kambi hiyo ya Huduma za Madaktari Bingwa wa Moyo itadumu siku tano ambapo siku ya kwanza ya zoezi hilo mwitikio wa wananchi walijitokeza ni takribani wananchi 120 lengo ni kuwafikia wagonjwa zaidi ya 800.
Dkt. Pedro Pallangyo Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo na mkuu wa idara ya tafiti ,mafunzo na upimaji afya kwa jamii kutoka Taasisi ya Magonjwa ya Moyo ya Jakaya Kikwete JKCI amesema dawa za kuongeza nguvu na nishati zimekuwa zikiathiri mfumo wa binadamu kufanya kazi hali inayopelekea kupanda kwa presha ,kiharusi na moyo kusimama ghafla .
Kwa upande wao baadhi ya wa wananchi hao frank na anna wamesema kwamba ujio wa huduma hiyo umekuja wakati muafaka kwani hivi sasa wananchi wengi wamekuwa wakitumia gharama kubwa kufuata matibabu hivyo wanaiomba serikali kuwe na utaratibu wa mara kwa mara kwa clinic hizo.