DC Mufindi akagua miradi ya maendeleo Mafinga
30 March 2024, 10:54 am
Miradi mingi ya maendeleo katika Halmashauri ya mji Mafinga imekamilikankwa asilimia 95 kutokana na kupokea fedha serikali kuu na fedha za ndani.
Na Hafidh Ally
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Dkt. Linda Salekwa amefanya ziara kukagua Miradi ya Maendeleo katikati Halmashauri ya Mji Mafinga.
Miradi iliyokaguliwa na kutembelewa ni Ujenzi wa Nyumba ya watumishi(2 in 1)katika Zahanati ya Kisada ambapo Jengo limekamilika kwa asilimia 95,Kituo cha Afya Bumilayinga ambapo sehemu kubwa kimekamilika.
Ukamilishaji unaendelea kwa jengo la kuhifadhia maiti,walkways na jengo la kufulia na ukamilishaji wa Mfereji wa umwagiliaji Katika Kijiji cha Mtula ambao mradi umekamilika kwa asilimia 95.
Akisoma taarifa kwa Mkuu wa Wilaya, Mganga Mfawidhi Zahanati ya Kisada Dkt. Atidius Filberti amesema ujenzi wa nyumba za watumishi( 2 In 1) uliibuliwa na wananchi na baadae Halmashauri ya Mji Mafinga ikaona juhudi za wananchi na kuweka kiasi cha shilingi milioni 60 kutoka mapato ya ndani kukamilisha mradi huu ambao tayari umekamilika kwa asilimia 98.
Akiwa katika ukaguzi wa Mfereji wa umwagiliaji Mtula Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ameagiza kulingana na fedha nyingi kuingizwa na Serikali katika mradi huu zaidi ya shilingi milioni 566 kutoka Serikali Kuu amewataka wataalamu kuhakikisha tija kubwa inapatikana kwenye mradi na wananchi wanalima mazao yenye tija kwa mwaka mzima bila kusahau kilimo cha Matunda na mboga mboga ili kupambana na udumavu.
Mfereji huu wa Mtula unasaidia wakulima na wananchi wa kijiji cha Mtula na ni mfereji wenye urefu wa kilomita 1.3 na mfereji huu haukauki Maji hivyo kufanya wakulima wa eneo hilo kulima mazao kwa mwaka mzima. MAZAO Makuu yanayolimwa kandokando ya mfereji huo ni mahindi maharage na mbogamboga.
Ziara imehudhuriwa na Mkurugenzi Mji Mafinga Bi. Fidelica Myovella pamoja na baadhi ya Wakuu wa Divisheni na Vitengo.