Wafugaji kutumia bidhaa za lishe kutoka YARA.
21 September 2023, 11:34 am
Na Adelphina Kutika
Wafugaji mkoani Iringa wametakiwa kutumia bidhaa ya Lishe ya wanyama kutoka Yara ili kuboresha mifugo yao na kukuza kipato kwa ufugaji.
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa mkoa wa iringa Halima dendego katika hafla ya uzinduzi wa bidhaa mpya za lishe ya mifugo kutoka kampuni ya Yara ambapo amesema wafugaji wote watumie bidhaa bora na zilizoainishwa na wataalamu wa lishe ya mifugo ili kuondokana na wajanja wanaouza bidhaa feki na hatari sokoni.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Yara Tanzania, Winstone Odhiambo amesema kampuni hiyo inayojihusisha na uagizaji na usambazaji wa mbolea hapa nchini hadi sasa ni kampuni tanzu ya Yara International ASA , ambayo inaongoza katika uzalishaji wa mbolea duniani na katika masuala ya utunzaji wa mazingira na lishe.
Mmoja wa wafanyabiashara wa bidhaa za kilimo Mkoani Iringa, Mkurugenzi wa Meja Agrovet Supply , Majorino Yangi alisema kuwa huduma hiyo hiyo imekuja kwenye wakati mwafaka na kuwaponyeza Yara kwa kuzindua rasmi Lishe ya Mifugo ambayo itasaidia wafugaji kukuza Mifugo Yao katika njia nyingine.
Nao baadhi ya wakulima wa mifugo mbalimbali mkoani Iringa wamesema wamekuwa wakipata changamoto za ulishaji wa Mifugo wakati wa kiangazi lakini ujio wa Yara utasaidia upatikanaji wa chakula kwa wingi
SAUTI 3 WAFUGAJI
MWISHO