Mbunge Midimu Aiomba Serikali kuwapatia Jokofu la Maiti na genereta Hospital ya Itilima.
18 April 2023, 2:10 pm
Hospital ya Wilaya ya Itilima imekuwa ikitoa huduma za afya kwa wananchi wengi huku ikibaliwa na changamoto ambazo serikali imeombwa kuzitatua.
Na Hafidh Ally
Hospitali ya Wilaya ya Itilima iliyopo Mkoa wa Simiyu inakabiliwa na Changamoto ya ukosefu Jokofu la kuhifadhia Maiti katika Mochwari pamoja na ukosefu wa Genereta.
Hayo yamezungumzwa Bungeni Jijini Dodoma na Esther Midimu Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu alipokuwa akichangia Hoja katika Wizara ya TAMISEMI na kuongeza kuwa wananchi wamekuwa wakipata shida ya kuhifadhi wapendwa wao pindi wanapofariki huku akiiomba serikali kutenga fedha za kutatua changamoto hiyo.
Akizungumzia kuhusu changamoto ya ukosefu wa Genereta Mh. Esther amebainisha kuwa Hospitali ya Itilima haina genereta jambo linalohatarisha usalama wa wagongwa wanaofanyiwa upasuaji endapo umeme utakatika ghafla.
Aidha Mh. Midimu ameiomba serikali kuwapatia fedha za kujenga uzio kwani kwa sasa wana wodi ambayo inalaza wagongwa jambo linalopelekea kuwa na usalama mdogo.
“Kwa kweli wagongwa wamekuwa na usalama mdogo kwa sababu Kuna changamoto ya kutokuwa na uzio kwani Kuna huduma ya wodi ya kulaza wagongwa” Alisema Mh. Midimu
Katika hatua nyingine ameiomba serikali kuwapatia watumishi wa afya katika vituo vya afya ambavyo vimejengwa ili kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.