Kabati aiomba Serikali Kufuta Kodi ya vifaa tiba.
14 April 2023, 4:59 pm
Kodi za vifaa tiba zinapelekea vifaa hivyo kuchelewa bandarini kutokana na kutokuwepo kwa mpango mzuri wa kuviruhusu ili vikatoe huduma kwa wagonjwa.
Na Hafidh Ally
Serikali imeombwa kuweka mpango mkakati wa kuondoa Kodi ya vifaa tiba kutoka Bandarini ili viweze kuwahudumia wagonjwa kwa wakati.
Hayo yamezungumzwa Bungeni Jijini Dodoma na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa Dkt Ritta Kabati Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi Cha maswali na majibu na kuongeza kuwa serikali haioni haja ya kuondoa tozo hizo kwani kumekuwa na changamoto ya kuwepo kwa mlolongo mrefu wa taratibu za kikodi ambazo zinasababisha wagongwa wasipate huduma za kitabibu.
Kabati alihoji kuwa vifaa tiba kama mashine za mionzi kukaa vimekuwa vikikaa muda mrefu bandarini huku akiiomba serikali pia kuweka utaratibu mzuri wa kuondoa kabisa Kodi katika vifaa tiba vya magonjwa ya kansa na Figo ili hospitali zote ziweze kutoa huduma hiyo kwa wagonjwa.
“Serikali ijitahidi kuweka mpango mkakati mzuri ili Vifaa hivyo viweze kufika kwa wakati na kusaidia wagonjwa mahututi” Alisema Kabati
“Serikali ijitahidi kuweka mpango mkakati mzuri ili Vifaa hivyo viweze kufika kwa wakati na kusaidia wagonjwa mahututi” Alisema Kabati
Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Hamad Hassan Chande amesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya Kodi ya ongezeko la thamani sura namba 148 Vifaa tiba, Kinga, na dawa vina sifa ya kupata msamaha wa Kodi na kuongeza kuwa endapo Waziri wa afya ataridhia, watafuta Kodi yake.