Tanroads Iringa yaicharaza Njombe 5-0
28 February 2023, 4:58 pm
Katika kujenga mahusiano mazuri ya kiutendaji,TANROADS mkoa wa Iringa pamoja na mikoa ya Njombe na Mbeya wamefanya bonanza la michezo.
Na Ansigary Kimendo
TANROADS mkoa wa Iringa wamefanya bonanza la michezo lililoshirikisha watumishi wa TANROADS kutoka mikoa ya Njombe Mbeya na mwenyeji akiwa ni Iringa lengo likiwa ni kufahamiana na kujenga mahusiano mazuri baina yao.
Bonanza hilo lililofanyika siku ya Jumamosi tar 25.02.2023 kwenye Viwanja vya Samora mkoani Iringa likijumuisha mchezo wa mpira wa pete kwa wanawake, na mpira wamiguu kwa wanaume, ambapo Katika mchezo wa Mpira wa Miguu TANROADS mkoa wa Iringa waliibuka na ushindi wa magori 5-0 dhidi ya TANROAD Njombe.Huku mpira wa pete TANROADS mkoa wa Mbea wakishinda mabao 20-3 dhidi ya Iringa.
Akizungumza mara baada ya Mchezo huo kumalizika mchezaji kutoka timu ya TANROADS mkoa wa Njombe HADSON MTAGILA amesema kuwa mchezo huo ulikuwa mzuri na licha ya kufungwa na wao waliweza kuhamasika kuanzisha mabonanza hayo.
Tumefungwa lakini tunashukuru tumeweza kufahamiana na imetupa hamasha
Akizungumza mara baada ya Mchezo huo kumalizika mchezaji kutoka timu ya TANROADS mkoa wa Njombe Hadson Mtagila amesema kuwa mchezo huo umekuwa mzuri na licha ya kufungwa na wao wameweza kuhamasika kuanzisha mabonanza hayo.“Tumefungwa kwenye mchezo wa miguu lakinitunashukuru tumeweza kufahamiana na imetupa hamasha nasisi kuanzisha mabinanza”
Feby Raban kutoka timu ya TANROADS mkoa wa Mbeya ameeleza namna alivyofurahia bonanza hilo kwa kutoa nafasi michezo mbalimbali ambayo imekuwa haipewi kipaumbele ikilinganishwa na mpira wamiguu hasa mpira wapete ambapo timu hiyo iliweza kupata ushindi wa mabao 20-3 dhidi ya Iringa.
Kwa upande wake ALEX MGONGOLWA ambae ni mratibu wa michezo kutoka TANROADS mkoa wa iringa alisema kuwa mambonanza hayo yatakuwa ni endelevu ambapo Tanroad mkoa wa Iringa watakwenda kushindana na mikoa mingine.