Simba, Yanga Na Azam Zatenganishwa Kombe La Mapinduzi
16 December 2022, 5:01 pm
MABINGWA watetezi, Simba SC wamepangwa Kundi C pamoja na Mlandege na KVZ katika michuano ya Kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza Januari 1 hadi 13, mwakani.
Kwa upande wao, mabingwa wa Bara, Yanga SC wao wapo Kundi B pamoja na Singida Big Stars na wenyeji, KMKM ambao pia ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Zanzibar.
Kundi A linaundwa na Azam FC ya Dar es Salaam, wenyeji, Malindi SC na Jamhuri FC ya Pemba, wakati Kundi D kuna Namungo ya Lindi, Aigle Noir ya Burundi na Chipukizi ya Pemba.
RATIBA KOMBE LA MAPINDUZI
Januari 1, 2023
Mlandege v KVS Saa 10:15
Malindi SC v Jamhuri Saa 2:15
Januari 2, 2023
Namungo v Chipukizi Saa 10:15
Singida BS v KMKM Saa 2:15
Januari 3,2023
Azam FC v Malindi SC Saa 10:15
Simba SC v Mlandege Saa 2:15
Januari 4, 2023
Chipukizi v Aigle Noir Saa 10:15
Yanga SC v KMKM Saa 2:15
Januari 5, 2023
Jamhuri v Azam FC Saa 10:15
KVZ v Simba SC Saa 2:15
Januari 6, 2023
Namungo v Aigle Noir Saa 10:15
Yanga SC v Singida BS Saa 2:15
Januari 8, 2023
NUSU FAINALI 1 Saa 2:15
Januari 9, 2023
NUSU FAINALI 2 Saa 2:15
Januari 13,2023
FAINALI Saa 2:15
(Nusu Fainali ya kwanza ni mshindi wa Kundi A dhidi ya mshindi Kundi B na ya pili ni mshindi wa Kundi C dhidi ya mshindi wa Kundi D).