Ukosefu wa maji kwa wananchi ilula
9 July 2021, 6:57 am
Wananchi wa kijijiji Cha Igingilanyi Kata ya Ilula Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa wako katika hatari ya kupata maradhi ya kuhara kutokana na kukosekana kwa huduma ya maji Safi na salama.
Wananchi hao wameiomba serikali kuwatatulia changamoto ya maji katika kijiji hicho kwani wamekuwa wakikumbana maradhi mbalimbali ya tumbo kwani maji hayo pia utumiwa na mifugo.
Wananchi hao wamesema kuwa wamekuwa wakiamka saa nane usiku ili kufuata maji katika visima na madimbi hayo kwa sababu muda huo maji yanakuwa yametulia kutokana na maji hayo kutumiwa na mifugo yao.
Aidha wananchi hao wameiomba serikali kuwatatulia kero ya maji katika kijiji chao kwani maji wanayotumia yana vijidudu ambapo wakati wa kiangazi huwa wanakosa kabisa maji hayo.
Naye Diwani wa kata ya Ilula ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya kilolo ANA MSOLA amesema mpango uliopo kwa sasa kutoka Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira IRUWASA ni kufanya ukarabati wa maji wa mabomba mara baada ya bajeti ya serikali kutoka.