Changamoto ya Ukosefu wa zahanati
21 June 2021, 4:05 pm
Wananchi wa kijiji Cha Ugute kata ya isalavanu Mkoani iringa wanakabiliwa na Changamoto ya Ukosefu wa zahanati jambo linalowafanya wafuate huduma za afya katika kijiji Cha Jirani
Wakizungumza na Nuru FM baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamesema kuwa Ukosefu wa zahanati unawafanya wasafiri kwenda kijiji Cha Jirani kwa ajili ya kupata huduma za afya huku wajawazito wakiwa wahanga wa changamoto hiyo.
Wamesema kuwa wako tayari kutoa eneo kwa ajili ya zahanati huku wakiiomba serikali kuwasaidia fedha pale watakapotenga eneo kwa ajili ya zahanati ya kijiji Chao.
Wamesema kuwa wanategemea zahanati ya kijiji Cha isalavanu ambayo hata hivyo haikidhi uhitaji wa wananchi wote.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji Cha Ugute Bw. Shija Kilufi amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo huku akiahidi kushirikiana na wananchi kuandaa mpango mkakati wa kuwa na zahanati yao.