”Serikari itutengenezee barabara”…..
8 June 2021, 9:06 am
Wananchi wa kijiji cha Kilosa Kata ya Ihanu Wilaya ya Mufindi Mkoani iringa wamelalamikia ubovu wa barabara katika kijiji chao jambo linalosababisha kukosekana kwa usafiri.
Aidha wanakijiji hao wameiomba serikali kuwarekebishia barabara ambayo ndio kitovu cha uchumi wa mkoa wa iringa kutokana na kijiji chao kutoa mbao kwa wingi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Kilosa Siadi Kalinga amekiri kuwepo na changamoto ya brabara, huku akiiomba serikali kuu kuwatatulia kero hiyo.
Wakizungumza na Nuru fm baadhi ya wananchi hao wamesema kuwa barabara ya kwenda kijiji kwao ni mbovu huku usafiri ukikosekana na hata ukipatikana nauli inakuwa ni kubwa.
Naye Mbunge Mbunge wa Jimbo la Mafinga kaskazini ambaye pia ni Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Mh. EXAUD KIGAHE amesema kuwa barabara hiyo iko katika kipaumbele chake hivyo wananchi wawe na subira wakati bajeti ya barabara hiyo ikiandaliwa