Wanabari pingeni ukeketaji
15 March 2021, 10:59 am
Waandishi wa habari wa redio za jamii nchini wametakiwa kuelimisha jamii juu ya kupinga ukeketaji na ndoa za utotoni dhidi ya wanawake na watoto
hayo yamezungumzwa na afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Arusha Angela Kiama Mvaa katika mafunzo ya siku mbili ya waandishi wa habari kuhusu ukeketaji kwa wanawake na watoto yaliyoandaliwa na shirika la C-Sema kwa kushirikiana na shirika la umoja wa mataifa UNFPA ambapo amewataka wanahabari kuwa sauti ya kukemea masuala hayo husasani maeneo ya vijijini.
WARREN BRIGHT ni afisa uhusiano wa UNFPA amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha wandishi wa redio jamii nchini wanapata mbinu bora za kuandaa vipindi dhidi ya ukeketaji kwa wanawake na watoto
KWA upande wake Michael Marrwa kutoka shirika la C-Sema amewataka wanahabari kuelimisha jamii juu ya ukatili kwa watoto kwa kuwa watoto huweka visasi na kuathirika kisaikolojia pia.