Nurufm washerehekea sikukuu ya wapendao
15 February 2021, 12:41 pm
Wafanyakazi wa Kituo cha Redio NURU FM kilichopo Manispaa ya Iringa wamesherehekea sikukuu ya Wapendao kwa kutembelea kituo cha Huruma Center ambacho kinalelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Akizungumza mara baada ya kutembelea Kituo hiko Afisa Utawala wa Nuru fm, Denisi nyali amesema kuwa wamefarijika kuwatembelea watoto hao na kupata nao chakula cha mchana ambapo pia waliweza kupata historia kituo hicho ambacho kimewasaidia watoto zaidi ya Mia nane.
Amesema kuwa Nuru fm kupitia vipindi vyake itazidi kuwahamasisha wananchi kuwajali watoto yatima na wanaoishi katika mazingira ili na wao waweze kuishi kama wanaoishi watoto wengine.
Kwa upande wake Mkuu wa kituo cha Huruma Center Mchungaji Joyce ngandango amesema kituo chao huwa kinapokea watoto wanaofanyiwa vitendo vya ubakaji huku wakiendelea kutoa kuwahudumia watoto wao.
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim gwada ambaye aliongozana na Wafanyakazi wa Nuru Fm amewapongeza kwa kuwatembelea Kituo hiko cha kuwalea watoto Yatima huku akiahidi kuwa halmashauri yake kushirikiana na Viongozi wa kituo hiko kuwahudumia watoto hao.
Kituo cha Huruma Center ambacho kinawalea watoto yatima na wale ambao wanaishi katika mazingira kimeweza kuwahudumia zaidi ya watoto mia nane toka kianzishwe.