Nuru FM
Nuru FM
9 April 2026, 09:03

Changamoto ya Maji na Barabara imetajwa kukwamisha shughuli za kimaendeleo kwa wananchi wa jimbo la Mafinga.
Na Fredrick Siwale
Wananchi wa Jimbo la Mafinga Mjini Mkoani Iringa wameiomba serikali kutatua changamoto ya Maji na Ubovu wa miundombinu ya barabara.
Wakizungumza katika Mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini, Mh. Dickson Lutevele VILLA, wananchi hao wamesema kuwa katika eneo la Lumwago kuna changamoto ya Barabara sambamba na changamoto ya Maji katika Mtaa wa Mkombwe.

Naye Diwani wa Kata ya Boma Mh. Baraka Kisakanike amesema kuwa Kata ya Boma imekuwa na changamoto ya ubovu wa barabara hasa katika kipindi hiki cha Mvua.
Akijibia changamoto hizo, mbunge wa Jimbo la Maafinga Mjini Mh. Dickson Lutevele VILLA amesema kuwa kuna mradi wa maji unatekelezwa utakaotoa lita Milion 11 kwa siku.
Kuhusu changamoto ya Barabara Mh. Villa amesema kuwa watashirikiana na Tarula na kuanza kufanya ukarabati wa barabara korofi mara baada ya mvua kupungua. MWISHO