Nuru FM

TAKUKURU yaokoa Mil 106 za Tanroad Iringa

2 March 2026, 5:19 pm

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Iringa, Victor Swela akizungumza na wanahabari. Picha na Ayoub Sanga

TAKUKURU ilibaini watu binafsi walikuwa wakijinufaisha kwa kukusanya mapato hayo kwa njia zisizo rasmi.

Na Ayoub Sanga

Jumla ya Shilingi milioni 106 zimepatikana kutokana na uboreshaji wa usimamizi wa makusanyo ya matumizi ya hifadhi za barabara mkoani Iringa, kufuatia hatua zilizochukuliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kushirikiana na Wakala wa Barabara (TANROADS).

Fedha hizo zimekusanywa katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2025 baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa kidijitali wa ukusanyaji mapato, uliolenga kuziba mianya ya upotevu wa fedha iliyokuwa ikisababishwa na baadhi ya watu binafsi kukusanya tozo hizo kwa utaratibu usio rasmi.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Iringa, Victor Swela, amesema TAKUKURU ilifanya ufuatiliaji maalum katika maeneo ya Ndiuka, Ifunda, Ilula, Mtua na Ruaha Mbuyuni, ambako ndipo changamoto za ukusanyaji zilipobainika.

Sauti ya Mkuu wa Takukuru

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mipango TANROADS Mkoa wa Iringa Mhandisi Michael Anyandwile , amefafanua kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Barabara Na. 13 ya mwaka 2007, TANROADS ilianza rasmi kusimamia maegesho ya magari katika kituo cha Ndiuka kuanzia Agosti 2025.

Sauti ya Michael

Kabla ya hapo, maegesho hayo yalikuwa yakisimamiwa na vikundi pamoja na watu binafsi, hali iliyosababisha Serikali kukosa mapato yaliyostahili ambapo kuanzisha matumizi ya Mfumo wa Malipo wa Serikali kwa njia ya namba ya kumbukumbu ya malipo (control number), mapato yaliongezeka kutoka takribani shilingi milioni 20 kwa mwaka hadi kufikia kati ya shilingi milioni 25 hadi 27 kwa mwezi.

Sauti ya Michael