Nuru FM
Nuru FM
10 February 2026, 3:42 pm

“Makundi ndio sababu ya kushindwa kuleta maendeleo kwa jamii, Tuyavunje tuwe wamoja”
Na Fredrick Siwale
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa wametakiwa kuvunja makundi waliyo kuwanayo wakati wa uchaguzi ili waweze kuwatumikia wananchi.
Hayo yamezungumzwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa MCC Salim Asas walipokuwa mgeni wa katika kikao Maalumu Cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Mufindi na kuongeza Kuwa makundi hayana faida Kwa Sasa na badala yake waungane kwa pamoja kutatua changamoto za wananchi.
“Yake makundi yaliyijitokeza wakati wa uchaguzi mkuu, na sasa ni muda wa kuvunja makundi yote Kwa sababu Tumehimizwa kuachana nayo, na haya makundi yakiendekezwa chama kitavunjika na lazina tuondoe majereha ya majina ya watu kukatwa” Alisema Asas

Awali Mwenyekiti wa wa CCM Wilaya ya Mufindi George Kavenuke amesema Kuwa wameshafanya vikao na Mikutano katika maeneo yote ya Wilaya ili kurudisha Ari ya utendaji kazi kuanzia ngazi ya shina na majimbo yote.
Naye Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini na Naibu Waziri wa Uchukuzi Mh. David Kihenzile amemshukuru Mjumbe wa Kamati Kuu Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa MCC Salim Asas kwa kusimamia vyema uchaguzi uliotamatika bila yeyote kujiusisha na rushwa.