Nuru FM
Nuru FM
4 December 2025, 5:52 pm

“Bati hizi ni utekelezaji wa ahadi ambayo niliitoa kwenu na naikabidhi rasmi hii leo”
Na Ayoub Sanga
Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Fadhil Ngajilo, amekabidhi mabati 100 kwa Wafanyabiashara wa Kuku katika Soko la Mlandege, kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa mabanda ya kuuzia kuku ambayo yalikuwa hayajafunikwa.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Mh. Ngajilo amesema hatua hiyo ni sehemu ya ahadi zake za kuboresha miundombinu ya masoko ndani ya Manispaa ya Iringa, ili kuwajengea wafanyabiashara mazingira salama na yenye tija kwa shughuli zao za kila siku.
Katika hatua nyingine, Mbunge Ngajilo amewasihi wafanyabiashara hao, hususan vijana, kuendelea kulinda amani, mshikamano na kufanya kazi kwa bidii, akisisitiza kuwa maendeleo ya soko na ustawi wa biashara zao unategemea utulivu na ushirikiano wa pamoja.

Kwa upande wao Wafanyabiashara wa kuku katika soko hilo wameeleza kuwa mabati hayo yatamalizia changamoto ya muda mrefu ya mabanda yasiyofunikwa, hali ambayo ilikuwa inasababisha usumbufu hasa nyakati za mvua na jua kali.