Nuru FM
Nuru FM
4 December 2025, 2:49 pm

“Tushirikiane katika kuwatumikia wananchi ili kuleta maendeleo”
Na Joyce Buganda
Diwani wa kata ya Nzihi Steven Mhapa amefanikiwa kutetea Nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa kwa kura 37 kati ya kura 37 zilizopigwa huku kiti cha makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo kikienda kwa Mheshimiwa Constantino Makala.
Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo ambao uliambata na kikao cha kwanza cha baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa mheshimiwa Steven Mhapa ameushukuru uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kuongoza halmashauri hiyo kwa kipindi cha miaka mitano kama mwenyekiti huku akisisistiza umoja na mshikamano uliokuwepo uendelee.

Anord Mvamba ni katibu itikadi na uenezi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa amempongeza mheshimiwa Mhapa kwa kuchaguliwa kwa kishindo na kusema ushindi huo unaonyesha ameamininwa na madiwani wenzie pamoja na wananchi wa wilaya hiyo.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mahuninga Michael Vahaye amesema ndani ya siku 100 za kwanza atajitahidi kushirikiana na wataalamu wa halmashauri na mbunge wake katika kusimamia na kumalizia miradi iliyokuwa haijamalizika.
Baraza hilo la kwanza kwa Halmaushauri ya Wilaya ya Iringa lilifanyika katika ukumbi wa makao makuu ya halmashauri hiyo uliopo ihemi ambapo sambamba na uapisho kwa madiwani na uchaguzi wa mwenyekiti na makamu wa halmashauri baraza hili lilijadili kamati mbalimbali kama mpango kazi wa mwaka 2025mpaka 2030.