Nuru FM

INEC yawaonya wasimamizi wa uchaguzi kuzingatia maadili

27 October 2025, 3:31 pm

Msimamizi wa Uchunguzi Jimbo la Mafinga Mjini Dorothy Kobelo akizungumza na wasimamizi wa vituo vya kupiga kura. Picha na Fredrick Siwale

“Zingatieni maadili na viapo vyenu mnapoenda kusimamia uchaguzi katika vituo vyenu”

Na Fredrick Siwale

Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Jimbo la Mafinga Mjini Imewataka Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa vituo vya kupigia kura kusimamia maadili na masharti ya uchaguzi katika maeneo yao.

Hayo yamezungumzwa na Msimamizi wa Uchunguzi Jimbo la Mafinga Mjini Dorothy Kobelo wakati wa mafunzo ya siku mbili ya kupiga kura kwa Wasimamizi na Wasimamizi wasaidizi wa Vituo vya kupigia kura ambapo INEC inaamini hawatakwenda kugeuka kuwa chanzo cha malalamiko kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Sauti ya Kobelo

Naye Peter Ngussa ambaye ni Msimamizi msaidizi wa Uchaguzi Jimbo la Mafinga Mjini, amewataka Washiriki kuheshimu uteuzi wao na kuwaeleza kuwa wameongeza CV hata ya kusema Waliwahi kusimamia zoezi la Uchaguzi Mkuu.

Sauti ya Ngusa

Ngusa amewataka wasimamizi, Makarani waongoza wapiga kura kutojihusisha na masuala ya kisiasa kwani wao ndio waajiriwa wa tume huru ya uchaguzi sambamba na kuwapa kipaumbele makundi maalumu.

Sauti ya Ngusa

Awali Msimamizi msaidizi wa Jimbo la Mafinga Mjini Charles Mwaitege amesema mafunzo hayo yameshirikisha Washiriki 645 maeneo mawili tofauti vya Changalawe Sekondari na Ukumbi wa Mwamnyange ambapo kuna Jumla ya Vituo ni 209 kwa kata zote 9 za Jimbo la Mafinga.