Nuru FM

Villa aahidi kutatua Kero ya Maji Mafinga

23 October 2025, 10:46 am

Mgombea wa Ubunge Jimbo la Mafinga Mjini Mh. Villa akizungumza na wananchi Kata ya Wambi. Picha na Fredrick Siwale.

“Nichagueni ili niwaletee huduma bora ya maji katika eneo lenu” Villa

Na Fredrick Siwale

Mgombea wa Ubunge Jimbo la Mafinga Mjini kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dickson Nathan Lutevele Villa ameahidi kutatua kero ya Maji kwa wananchi wa eneo la Soko jipya Pipe line Kata ya Wambi.

Akizungumza wakati wa kunadi sera na kuomba kura za udiwani, Ubunge na Urais kuelekea uchaguzi mkuu wa Oct 29, Villa amesema kuwa atahakikisha wananchi wa eneo hilo wanapata huduma ya maji ambayo itawasaidia pia kufanya shughuli za kilimo.

Sauti ya Villa

” Nimekuja kuomba kura za Dkt. Samia Suluhu Hassan mgombea Urais mteule kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwangu nafasi ya Ubunge jimbo la Mafinga Mjini na Udiwani Frank Kalinga kata ya Wambi.” Alisema Lutevele.

Aidha Villa amebainisha kuwa atahakikisha anashirikiana na Watumishi wa Umma Mjini Mafinga kuwatumikia na kuwashirikisha Wananchi pale wanapokutana na changamoto katika shughuli za ujasiriamali.

Sauti ya Villa

Kwa Upande wake Mgombea wa Udiwani kata ya Wambi Kupitia CCM Frank Kalinga pamoja na kuomba kura, alieleza vipaumbele vyake vitatu katika eneo hilo ili kuisaidia Jamii ikiwemo kuwajengea banda la kufanyia biashara.

Kalinga amesema katika eneo hilo ipo changa moto ya banda la Soko jipya, mikakati ya utunzaji vyanzo vya maji na changamoto ya maji katika eneo hilo.

Sauti ya Kalinga