Nuru FM
Nuru FM
17 October 2025, 8:20 am

Nuru FM kupitia Kampeni yake ya ulipo tupo imeendelea kufanya matukio ya kijamii kuelekea katika kilele cha miaka 17 toka kuanzishwa kwake.
Na Hafidh Ally
Kuelekea kusherehekea Miaka 17 toka Nuru fm Radio ilipoanishwa, Wafanyakazi wa Kituo hicho wametembelea hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa kwa ajili ya kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo, Meneja wa Nuru Fm Gerald Malekela amesema kuwa vifaa hivyo ni pamoja na Magongo ya kutembelea, Maji, sabuni na dawa za meno huku akiwashukuru pia shirika la IDYDC kwa kushirikiana nao kutekeleza jambo hilo.

Aidha ameushukuru uongozi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana nao katika kuhakikisha taarifa za hospitali zinawafikia wananchi wote kwa wakati.
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa Dk. Iddi Omary amewashukuru Nuru Fm Radio kwa kufika na kutoa msaada huo hasa magongo ambayo yatawasaidia wenye uhitaji.
Hata hivyo baada ya kukabidhi mahitaji hayo, wafanyakazi hao walipata fursa ya kutembelea vitengo mbalimbali katika hospitali hiyo kwa ajili ya kujionea jinsi wanavyotoa huduma za afya kwa wananchi.